HOME

Friday, November 16, 2012

ABDULHAMAN KINANA ACHAGULIWA KUWA KATIBU MKUU WA CCM

Mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi NEC mjini Dodoma, umempitisha Abdulhaman Kinana kuwa katibu mkuu wa chama hicho tawala.


Tayari Rais Kikwete ameshamteua Katibu Mkuu wa zamani, Philip Mangula, kuwa Makamu Mwenyekiti, akirithi mikoba ya Pius Msekwa.Jina la Kinana lilikuwa likitajwa mara nyingi kupita kwenye wadhifa huo.

Naye Mwigulu Nchemba amechaguliwa kuwa naibu katibu mkuu wa chama hicho upande wa bara na Vuai Ali Vuai upande wa Tanzania visiwani.

Wengine waliofanikiwa kupita kwenye secretarieti ya chama hicho ni pamoja na Asha Rose Migiro ambaye amechaguliwa kushughulikia masuala ya kimataifa na Zakhia Meghji amechaguliwa kushika nafasi ya uweka hazina.

Nape Nnauye ameendelea kushikilia nafasi yake katibu na uenezi wa chama hicho.

No comments:

Post a Comment