HOME

Saturday, November 17, 2012

BONGO MOVIE WAJIPANGA KUCHAGUA VIONGOZI WAPYA


Bongo Movie inatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wake ambao wataweza kuliongoza gurudumu la filamu kusonga mbele zaidi kutokana na kuwepo na taarifa kuwa viongozi waliopo ni wabinafsi na wanajinufaisha wenyewe.

Kwa mujibu wa katiba ya Bongo Movie viongozi hukaa madarakani kwa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mpya ambapo viongozi waliopita huruhusiwa kugombea tena.


Kwanza sisi tuna katiba yetu ambayo inaendesha klabu yetu kwahiyo katiba yetu moja ya vipengele ni namna ya uchaguzi, uongozi unakaa madarakani kwa muda wa mwaka mmoja kwahiyo inapofika lazima sheria ifuatwa ndio maana tunafanya uchaguzi mwishoni mwa mwezi huu na kikao cha kujadili uchaguzi huo utafanyia wapi tutajadili Jumanne tarehe 20 wiki ijayo, “mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Bongo Movie ya uchaguzi Jimmy mafufu

Viongozi ambao wapo madarakani, mwenyekiti alikuwa JB, makamu wake Athumani Mbilinyi, katibu ni Claud na Jackline Wolper lakini mweka hazina ni Richie Richie na Vicent Kigosi alikuwa ni msaidizi wake, lakini hii haimaanishi kwamba wanatoka, wanarusiwa tena kugombea wala katiba haiwafungi,”aliongeza.

“Nashukuru Mungu kwasababu wamechukua hizo form na kwa yoyote mwenye kuHitaji form ya uongozi anaweza akawasiliana na Bongo Movie ili apate form ya uongozi.”


No comments:

Post a Comment