HOME

Friday, November 30, 2012

"NINGEPENDA KUFANYA MAPENZI NA JUSTIN BIEBER".....Ke$ha

Hisia za mapenzi ni kama kikohozi, kuna wakati inabidi tu kufunguka. Hiki ndicho alichokifanya ‘Tik Tok hitmaker’ mrembo Ke$ha, ambae amesema angependa kutoka out na Justin Bieber na kufanya chochote kile ambacho kinaruhusiwa kisheria kufanywa na watu wenye umri zaidi ya miaka 18.


Japo kuwa Ke$ha aliwahi kukataa kuwa alishawahi kufanya mapenzi na Justin Bieber siku za nyuma, sasa amesema ingekuwa ni hivi karibuni ingekuwa poa sana tu kwa sababu Bieber yuko single na umri unamruhusu.


Alipoulizwa katika interview na Rolling Stone kama yuko tayari sasa hivi, nae akauliza kwa maringo, “wait, yuko halali kisheria? Naweza kwenda jela kwa sababu hiyo? "


Akimaanisha umri wa Bieber kama unatosha kufanya yote hayo kisheria. Na baada ya kuambiwa kweli Bieber ana miaka 18 sasa hivi ndipo alipofunguka ya moyoni.

Bieber

“Ok, then , ningeweza. Tungeweza kutoka na kununua lottery tickets, ku-vote, kucheza putt-putt golf. Kila kitu ambacho kinakubalika kisheria kufanyika katika umri wa miaka 18.”


Mtangazaji alipomwambia kuwa mchezo wa putt-putt golf unaweza kuchezwa na watu wa rika zote, mrembo huyo alijibu, “ kwenye Tennessee unaweza. Wanachukulia serious kweli. Lakini unaweza kuolewa na cousin yako-nadhani hii ni halali kwa umri wowote.” Hapo ameeleweka mrembo huyo aliyeongea kimafumbo kidogo.


Kwa upande wa Bieber bado haijafahamika rasmi kama ni kweli yuko single na ameachana na girlfriend wake Selena Gomez kwa sababu bado wanaonekana mara kadhaa pamoja ikiwa ni pamoja kuhudhuria after-party ya American Music Awards 2012.





No comments:

Post a Comment