HOME

Tuesday, December 18, 2012

AY amsainisha Stereo kwenye kampuni yake, Unity Entertainment

Kampuni ya AY, Unity Entertainment inaendelea kuongeza wasanii wa kuwasimamia baada ya hivi karibuni kumuongeza rapper Stereo kwenye roaster yake.

Tayari Unity Entertainment inasimamia kazi za Ommy Dimpoz na Feza Kessy.

Akiongea na 255 ya Clouds FM jana, Stereo ambaye awali alikuwa chini ya studio ya MLAB, alisema amejisikia fahari kuchukuliwa na AY kwenye kampuni yake na ni ndoto yake ya siku nyingi.

Alisema mkataba na kampuni hiyo aliusaini tarehe 12/12/2012 chini ya usimamizi wa mwanasheria Anna Mwakatundu.
Amesema mkataba huo utahusisha kurekodi nyimbo, kufanya video, promotion na mambo mengine kuhusiana na yeye.

“Ni ndoto yangu ya siku nyingi sana kufanya kazi na Ambwene,” alisema Stereo.

“Nilikaa naye chini nikazungumza naye tukaoa kuna kila sababu ya kufanya kazi pamoja na nimefurahia hatua hiyo coz ni kitu ambacho nimekuwa nikikidream siku nyingi sikuwahi kujua hata kaa itafika hapa. Wajua mtu ambaye amewahi kukuinspire once katika maisha yako ya muziki halafu kesho anakuja kuwa bosi wako.”


No comments:

Post a Comment