HOME

Saturday, December 15, 2012

HUSSEIN MACHOZI NA CPWAA NDANI YA NGOMA MPYA YA " READY TO GO".....


Katika mlolongo wa kazi za wasanii za funga mwaka ambapo kila msanii anafanya kila awezalo ili kutoa wimbo mpya, muunganiko Hussein Machozi pamoja na mkali wa Mission 12 O’clock, Cpwaa unaingia katika orodha hiyo.


Kutokana na fununu tulizopata ni kwamba wawili hao wamekwisha kamilisha kupika ngoma kali iitwayo “Ready To Go”.

Kazi hiyo imepikwa na producer Jayyson katika studio za Hip Palace Records kutoka kipande cha K’Nyama Dar es Salaam.Hussein Machozi amempa shavu CP kutokana na touch zake adimu na ambazo Hussein baada ya kufikiri sana aliona ndio zinafit kwa kazi hiyo.

“Ready To Go” inakaribia kudondoka kwenye vyombo vya habari ndani ya muda usiopungua wiki moja sasa na matayarisho yake yanatoa kila sababu ya kuamini kuwa itakuwa ni Hit. Zawadi nyingine ya Krismasi kutoka kwaa Machozi.


No comments:

Post a Comment