Pop star Rihanna ametoa msaada wa dola milioni 1.75 (zaidi ya shilingi bilioni 2) kwa hospitali iliyopo visiwani kwao Barbados kama kumbukumbu ya marehemu bibi yake.
Staa huyo mwenye miaka 24 amesema zawadi hiyo itakayotumika kununua vifaa kwaajili ya kansa kwa hospitali ni njia yake ya kurudisha fadhila kwa Barbados.
“Naamini kuwa hii italeta mabadiliko makubwa kwa watu wa Barbados. Hii imefanyika kuokoa maisha ama walau kuyaongeza.”
Bibi yake Rihanna, Clara “Dolly” Braithwaite alifariki mwezi June na ugonjwa wa kansa.Kutokana na msaada huo, kitengo cha radiotherapy katika hospitali hicho kimepewa jina la ‘Clara Braithwaite Center for Oncology and Nuclear Medicine’.
Wakati wa kutoa msaada huo Rihanna ambaye jina lake halisi ni Robyn Fenty alisindikizwa na mama yake Monica na babu yake Lionel Braithwaite.
No comments:
Post a Comment