HOME

Monday, December 17, 2012

Sajuki anahitaji maombi yetu, leo anaelekea India kwa matibabu

Leo muigizaji wa filamu nchini Sadick Juma Kilowoko aka Sajuki anaelekea nchini India kwaajili ya matibabu ya ugonjwa unaomsumbua. Hivi karibuni muigizaji huyo alikuwa akifanya matamasha katika mikoa mbalimbali ili kukusanya fedha kwaajili ya kugharamia matibabu yake.

Alitakiwa awe ameenda nchini humo tangu December 6 lakini fedha ilikuwa bado haijakamilika. Hivi karibuni akiwa jijini Arusha hali yake ilibadilika ghafla baada ya kuzidiwa usiku alipokuwa ameenda kwenye tamasha la kuchangisha fedha.

Hali yake ilibadilika ghafla baada ya wasanii wenzie wa Bongo Movie kumtaka aahirishe show yake ya jana Jumapili kwakuwa wao walikuwa na show nyingine juzi yake.

“Kwakweli kitu kama hicho kilituumiza sana, kilimuumiza sana Sajuki,” alisem Dinno ambaye ni rafiki yake Sajuki baada ya wasanii wa Bongo Movie kuwapa taarifa hiyo.

“Kiukweli baada ya hapo hali ya Sajuki ikabadilika. Siku ya kwanza tulilala vizuri. Siku ya pili tu ndio likaanza balaa. Kiukweli mimi nilikuwa nimelala kama saa kumi usiku ama saa tisa Wastara namkuta mlangoni analia ananiambia Sajuki kazidiwa sana. Kwenda kweli namkuta Sajuki yupo kwenye hali nyingine tofauti, anahemea juu, mapigo ya moyo ya juu, anapiga kelele. Sijawahi kumuona Sajuki akilia. Sajuki alikuwa analia ananiambia, ‘Dinno naumia sana, mimi nahisi nakufa sasa hivi’. Akaomba simu aongee na mama yake. Kwakweli maneno aliyokuwa akisema Sajuki ni maneno ambayo yaani mtu yeyote aliyekuwa anasikia angesema kweli yupo kwenye hali tofauti. Kweli Sajuki aliumwa siku hiyo, sikulala akawa ananiambia ‘mgongo unauma Dinno ni kama unawaka moto yaani kifua kinauma, sielewe ni nini.”

Hali yake bado si nzuri hivyo anahitaji maombi na sala.

No comments:

Post a Comment