HOME

Thursday, January 3, 2013

JIHADHARI NA WEZI WANAOCHANGISHA FEDHA ZA MSIBA WA SAJUKI


Kwa mujibu wa Steve Nyerere ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya mazishi ya marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia jana, kumejitokeza watu wanaojifanya kutumwa na familia kuchangisha fedha kwa njia ya simu.


Steve amesema kuna mtu mmoja anayetumia jina kubuni Tumaini ameendelea kukusanya fedha nyingi kutoka kwa watu mbalimbali na kusema kuwa waache mara moja kwakuwa ni mwizi.

Steve amekielezea kitendo hicho kama wizi usio na aibu kwa familia ya Sajuki iliyopo kwenye majonzi makubwa.

Ameongeza kuwa taratibu zote za kukusanya fedha zinaendelea msibani maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam huku yeye na Mike Sango wakihusika na ukusanyaji huo.

No comments:

Post a Comment