HOME

Sunday, January 6, 2013

P SQUARE WAAPA KUTOKANYAGA TENA ARDHI YA UGANDA....

Licha ya kupiga show ya nguvu mjini Kampala, Uganda mwezi uliopita, wasanii wa kundi la P-Square wamedaiwa kuapa kutokanyaga tena ardhi ya Uganda kwaajili ya show.

Uamuzi huo wameuchukua baada ya kudaiwa kushikiliwa kwa masaa kwenye hoteli ya nyota 5 waliyokuwa wamefikia kwa kushindwa kulipa bili.


Waandaji wa show hiyo walikataa kulipa bili hiyo kutokana na kuwa kubwa mno.Kwa mujibu wa vyanzo, mapacha hao Peter na Paul walisaini mkataba na mapromota hao na walilipwa gharama ya kufanyia show huku zile za malazi na usafiri zikiachwa.

Hata hivyo kulikuwa na kiwango cha mwisho ambacho wasanii hao walitakiwa kukitumia pale walipofikia lakini walizidisha na hivyo waandaji kuwataka walipe wenyewe na hivyo kuleta mgogoro mkubwa.

Wasanii hao wa Alingo walichukizwa na kitendo hicho na sasa wameahidi kutoenda nchini Uganda tena!!

No comments:

Post a Comment