HOME

Sunday, January 6, 2013

SAKATA LA WACHUNGAJI WAWILI MASHOGA WALIOKAMATWA NIGERIA.

Moja kati ya stori zinazomiliki headlines sasa hivi Nigeria ni hii ya wachungaji wawili mashoga kushitakiwa kwa kosa la kumlazimisha mwanaume mwenzao kufanya nao hayo mapenzi ya jinsia moja.

Wachungaji wenyewe ni Prince Ejimole (26) na Lawrence Udo (25) ambao walikamatwa na polisi wakiwa kwenye chumba cha hoteli.

Mchapo kamili umeanzia pale muumini wao mmoja alipoomba msaada wa kufanyiwa maombezi ambapo wachungaji hao walimualika kwenye chumba cha hoteli ambayo siku zote ndio wamekua wakifanya hayo mambo yao kwa siri.

Muumini aitwae Chidiebere ambae ni mwanaume alipofika chumbani hotelini badala ya kuanza kuombewa akajikuta akipapaswa kimahaba na mmoja kati ya wachungaji hao ambae alianza kumvua nguo mpaka kumshika kwenye sehemu zake za siri.

Chidi alipoona hivyo akapiga kelele na kuita uongozi wa hoteli ambao nao waliwaita polisi waliokuja kuwakamata wachungaji hao, wahudumu wa hoteli hiyo hawakua wameushtukia mchezo kwa sababu siku zote wachungaji hao wanapokuja kukodi chumba wanajua wamekuja kwa ajili ya maombi manake hata kelele za maombezi huwa wanazipiga.

Kesi yao tayari iko Mahakamani na itasomwa tena january 7 2013.

1 comment: