HOME

Monday, June 3, 2013

Malawi: Tunapinga Tanzania kupeleka Meli Ziwa Nyasa (Malawi).

 

Nchi ya Malawi imepinga na kulalamika kuhusiana na kusudio la Tanzania kupeleka meli mbili za abiria katika ziwa Nyasa na kudai, kitendo cha kufanya hivyo kitaadhiri na kutishia mazungumuzo yanayotafuta suruhisho la muda mrefu ili kulimaliza mzozo wa ziwa Nyasa (malawi) uliodumu kwa muda mrefu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Efraimu Chiume alikaririwa jumamosi akisema, kwamba viongozi wa juu wa serikali ya Tanzania walisikika hadharani wakisema kwamba serikali ina mpango wa kununua meli sita na mbili zitapelekwa ziwa Malawi kusaidia kuondoa tatizo la usafiri.

Waziri Chiume alidai mpango wa kupeleka meli ziwa Nyasa (malawi) umekuja katika hali ambayo siyo mwafaka ikichukuliwa kuwa mazungumzo yalikuwa yanaendelea bila matatizo.

Maofisa wa serikali ya Tanzania hawakuweza kupatikana kuliongelea swala hili.

Malawi ambayo iko upande wa magharibi mwa ziwa inadai kumiliki nusu yote ya upande wa kasikazini mwa ziwa na huku Tanzania ambayo iko upande wa mashariki nayo ikidai kumiliki nusu ya upande wa kaskazini ya ziwa wakati nusu ya kusini mwa ziwa ikimilikiwa na Malawi na Msumbiji kwa pamoja.

Mwezi uliopita malawi ilirudi kwenye mazungumzo ambayo mwanzo ilijitoa baada ya kuilalamikia Tanzania kwa kuwatisha wavuvi wa Malawi, madai ambayo Tanzania iliyakanusha.

Mzozo kwa kiwango kikubwa umesababisha kukwama kwa utafutaji wa gesi asilia na mafuta katika ziwa Nyasa.

Mwaka jana serikali ya Malawi iliiruhusu kampuni ya Kiingereza inayoitwa Surestream Petroleum kuanza kutafuta mafuta.

No comments:

Post a Comment