HOME

Thursday, November 15, 2012

"NAMPENDA AMINI KAMA RAFIKI YANGU LAKINI HATUNA UHUSIANO WOWOTE WA MAPENZI"....LINAHNA UHSIANO

"NAMPENDA AMINI KAMA RAFIKI YANGU LAKINI HATUNA UHUSIANO WOWOTE WA MAPENZI"....LINAHNA UHSIANO





Siku za hivi karibuni Amini na Linah ambao wamewahi kuwa wapenzi na hatimaye kuachana, wamekuwa karibu mno kiasi cha watu kuanza kuulizwa maswali kama wamerudiana tena. 

Leo November 15 wanaachia wimbo wao mpya waliofanya pamoja na ambao waliurekodi siku ya kuzaliwa ya Amini October 30.

Katika fainali za BSS zilizofanyika Ijumaa iliyopita,Amini na Linah waliimba pamoja na kushangaliwa mno kutokana na jinsi walivyokuwa wakiimba kama mtu na mpenzi wake.

Ukweli ni upi? Wamerudiana ama ni marafiki tu? Tumewatafuta na kufanya nao mahojiano mahsusi ili kuyarusha leo siku wanayoachia wimbo wao ili wauseme ukweli.

Katika mahojiano haya Linah ameanza kwa kusema kuwa lengo la wao kufanya wimbo wa pamoja ni kukata kile anachokisema ‘kilimilimi’ cha watu kuwa yeye na Amini hawazungumzi tena baada ya kuachana. “Kulikuwa na maneno mengi sana kwamba mimi na Amini hatuelewani, hatupatani, hatuna mawasiliano mazuri,” anasema Linah.“Lengo kubwa la sisi kufanya hivyo vitu kwa pamoja ni kuwadhihirishia kuwa bado tunapendana (anacheka na kumuuliza Amini) Kwani ni Uongo? Amini anajibu, “Hakika unenalo ni sahihi”. Linah anaendelea, “Hakuna ukweli wowote kuwa tumerudiana au lah! Sababu kila mtu anafanya mambo yake na tunafanya kazi kama kawaida japokuwa upendo bado uko pale pale.”

“Tutazidi kuendelea kuwepo kwasababu hatukugombana, hatukukorofishana, hatujawahi kutukanana hata siku moja mawasialiano yako vizuri tu, “anasema Amini.

No comments:

Post a Comment