HOME

Monday, December 17, 2012

Aslay kuurekodia wimbo wake mpya ‘Wahenga’ nchini Kenya

Mkurugenzi wa TMK Wanaume Family, Said Fella hivi karibuni alikiambia kipindi cha Friday Night Live cha EATV kuwa Aslay yupo busy nchini Kenya akirekodi wimbo wake mpya.

Fella amesema wimbo huo uitwao Wahenga utatoa funzo kwa jamii nzima na asilimia kubwa ni vijana kwakuwa unahusu hekima za wazee katika jamii ambapo Ally Nipishe wa THT ameshirikishwa.

Aliongeza kuwa anaamini Aslay anaendelea kufanya vizuri katika gemu na ndio alichaguliwa kuwania tuzo za KORA na kwamba huu ni muda muafaka kwake kufanya mambo makubwa.

Ili kubadiisha ladha ya muziki wake na kupambana na ushindani kimuziki aliamua kwenda kufanya wimbo wake mpya nchini Kenya.

Katika tuzo za Kora 2012 Aslay ametajwa kwenye kipengele cha ‘Best male newcomer’ na wimbo wake ‘Niwe Nawe’ akipambana na Floby Saanida (Burkina faso), Loyiso-Wrong to u, Frique du sud, Aziz Azion-My oxyen (Uganda), Davido Dami duro (Nigeria) na John chit wapusuku (Zambia)

No comments:

Post a Comment