Shirika la utangazaji la Uingereza, BBC leo litamtangaza mchezaji bora wa mwaka 2012. Wachezaji watano wanawania tuzo hiyo ambao ni Yaya Toure na Didier Drogba kutoka Ivory Coast, Demba Ba kutoka Senegal, Younes Belhanda wa Morocco na Naodha wa Zambia Christopher Katongo.
Wachezaji hao watano wameonyesha mchezo mzuri mwaka huu na wanne kati yao waliongoza vilabu vyao kushinda mataji mbali mbali.
Drogba alimaliza mkataba wake na klabu ya Chelsea kwa kufunga bao la ushindi lililoipa Chelsea ushindi katika fainali ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya, kwa mara ya kwanza na pia kufunga bao ambalo liliisaidia Chelsea kushinda kombe la FA.
Yaya Toure, amekuwa nyota wa Klabu ya Manchester City ambayo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 44, ilinyakuwa kombe la ligi kuu ya England.
Nchini Morocco, Belhanda aliongoza klabu yake kushinda kombe la ligi kuu na alifunga magoli 12 na klabu yake ya Montepilla, ambao ni mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa.
Barani Afrika, Chris Katongo aliongoza timu ya taifa ya soka ya Zambia kushinda kombe la mataifa bingwa barani Afrika. Vijana hao wa Chipolopo waliishinda timu ya taifa ya Ivory Coast kwenye fainali hizo
Jay Jay Okocha kutoka Nigeria ndiye mchezaji wa pekee ambaye amewahi kushinda tuzo hiyo kwa miaka miwili mfululizo mwaka wa 2003 na 2004.
No comments:
Post a Comment