Saturday, December 15, 2012

HUU NDIYO MKWANJA ANAOINGIZA JACK WA CHUZI KUPITIA FILAMU

Kama ni mpenzi wa kucheki filamu za Kibongo, haina shaka utakuwa unaifahamu orodha ndefu ya mastaa wa kike wanaofanya vizuri kwenye tasnia hiyo.

Kwenye exclusive interview aliyofanya na mtandao huu mwishoni mwa wiki iliyopita staa wa Jumba la Dhahabu, Jaclyn Pentezel ‘Jack wa Chuzi’, amefunguka kuwa sasa anajihisi milionea kufutia mshiko havi anaingiza kwa mwaka kupitia uigizaji.

Jack Wa Chuzi ‘super star’ wa muvi asiyekaukiwa matukio ameiarifu mpekuzi kuwa sasa anauhakika wa kuingiza kiasi cha shilingi za kibongo milioni 18 kwa mwezi kupitia malipo ya shilingi milioni 6 kwa kila muvi anayoigiza.

“Kwa sasa mtu akija na kazi yake sichezi chini ya shilingi milioni 6, ni kiwango ambacho ninaamini kiko kwenye hadhi yangu, ninafuraha kwa sababu sasa najihisi milionea” alisema Jack wa Chuz.

Akiendelea zaidi Jack alisema kuwa sasa anauhakika wa kumiliki milioni 360 kwa mwaka endapo ratiba yake ya kucheza muvi 3 kwa mwezi haitabadilika.
Huo ndiyo umilionea wa Jack wa Chuzi.

No comments:

Post a Comment