Saturday, December 15, 2012

"NTAFANYA KILA NIWEZALO ILI NIMUUE JACK WA CHUZI"...JACOB

MAISHA ya msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ yako hatarini kufuatia ujumbe wa kumuua unaosambazwa na muongoza filamu, Mandela Nicholas ‘Jacob’ anayedai kudhulumiwa na msanii huyo kiasi cha shilingi 325,000.

Kwa mujibu wa ujumbe huo, jamaa huyo amedhamiria kumfanyizia Jack kwa kumcharanga mapanga kisa eti kadhulumiwa kiasi hicho cha fedha ambazo ni malipo ya kumuongozea filamu yake.


Jacob anadai kuwa, awali alimuandikia ‘script’ na kumuongozea filamu msanii huyo lakini kabla kazi haijaisha, wakazinguana hadi kufikishana katika Mahakama ya Mwanzo Ilala jijini Dar.

Hata hivyo, mahakama alimuamuru Jack alipe fedha hizo lakini kinyume chake msanii huyo akawa mgumu kutekeleza, hivyo kwa hasira Jacob akamuandikia Jack sms hiyo ya vitisho.

Sehemu ya ujumbe huo inasomeka hivi; “Labda kifo kiniite leo Jack nitamuua, kama laki 325,000 hajanipa mtasikia. Kama rafiki au ndugu jiandae na mazishi ya marehemu Jk Pentzel full panga tu.”

Sehemu nyingine ya ujumbe huyo ilisomeka hivi;

“Wapendwa Jack anachohitaji sasa ni kifo na nitamuua kweli, mimi simsukumi…ila mapanga tu ndiyo dawa yake.
“Utapeli utamuua Jaki, leo kesho, keshokutwa mkisikia msiba ulizia kapigwa panga au? Kama siyo panga siyo Jacob, kama panga na vipande 150 ewaa. Yeye kaburini mimi Segerea. Jasho la mtu haliliwi.”

Akizungumza na mwandishi wetu kuhusiana na sms hiyo, Jack alisema kuwa naye ameipata na katika kujihakikishia usalama wa maisha yake amekwenda kuripoti polisi na kupewa RB.

No comments:

Post a Comment