VIBAKA WALIKATA KIDOLE CHA SHARO MILIONEA NA KUTAMBAA NACHO.....
Sharomilionea.
Siku kadhaa baada ya marehemu msanii sharomilionea kuzikwa, vile vitu ambavyo vilisemekana kupotea ama kuibiwa wakati wa ajali vimeanza kupatikana.
Akithibitisha habari za kupatikana kwa vitu hiuvyo, swahiba wake wa karibu ambaye alikuwa akiishi na Sharomilionea Kitale amesema amepata taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji kule Muheza Tanga kwamba baadhi ya vitu vimepatikana.
Kwa mujibu wa maelezo yake, vitu ambavyo vilikuwa vimeibwa ni pamoja nasimu mbili aina ya Blackberry na Samsung, Viatu, Cheni, tairi la spea ya gari, Betri, Radio ya gari na shilingi milioni sita taslimu ambazo alikuwa akimpelekea mama yake.
Bwana kitale aliendelea kwa kusema, cha kusikitisha zaidi katika tukio hilo la wizi, ni unyama uliofanywa na wezi hao ambapo baada ya kushindwa kumvua pete kwenye kidole cha msanii huyo, waliamua kumkata kidole na kuondoka na pete hiyo.
Aidha alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa alizonazo kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji kuna wanakijiji wamerudisha baadhi ya vitu kama Simu ya Mkononi,Pete,Cheni, Jeans, T-shirt,Viatu, ambapo walisema wamerudisha baada ya kugunduliwa na wanakijiji wenzao ambao walitoa taarifa baada ya kugundua vitu walivyokuwa navyo ni mali ya marehemu msanii Sharomilionea.
Kitale alisema “kuna kijana mmoja anayeitwa David ambae ni ndugu na mwenyekiti na wenzake ambao walitajwa na wanakijiji wenzao kwa kuhusika yeye pamoja na wenzake kufanya kitendo hicho ya bila kujua wanao mfanyia alikuwa ni Sharro baada ya kutambua watu hao wakafanya ionekane vitu hivyo vimepatikana kutoka kwa wanakijiji."
Kitale alimalizia kwa kusema kwa sasa vitu ambavyo havijapatikana ni pamoja na Betri, Tairi la spea, Radio ya gari na pesa ambazo anasema suala hilo tayari lipo poilisi kwa uchunguzi zaidi.
Hata hivyo habari zilizotufikia zinadai kuwa Watu wanne wamekamatwa na Jeshi la Police kwa tuhuma hizo za za kumkata vidole na kumuibia marehemu Sharo Milionea baada ya kupata ajali ya gari
No comments:
Post a Comment