"NITAUFUNGA MWAKA KWA TAMTHILIA YA HIGH HEELS....MASHABIKI WAKAE MKAO WA KULA"....MR.CHUZ
MSANII anayefanya vizuri kwenye upande wa filamu na tamthilia bongo, Mr Chuzi, ameuambia mtandao huu kuwa wanatarajia kufungua mwaka 2013 na tamthilia yao nyingine inayokwenda kwa jina la ‘High Heels’, ambayo itashirikisha wasanii wale wale waliofanya vizuri tamthilia zake zilipita.
Akiongea na mtandao huo Mr. Chuzi alisema kuwa mara huwa anapanga mipango ya mbali na tayari ameshajua mwakani mashabiki wa tamthilia zake wanataka nini hivyo ujio wa ‘High Heels’ utakuwa wa kipekee kabisa.
Alisema kuwa baada ya hiyo kutoka huku mashabiki wake wakiendelea kuitazama atakuwa kwenye mchakato mwingine wa kuipeleka sokoni filamu yake, ambayo bado haijakaa sawa kutokana na matatizo yaliyokuwa nje ya uwezo wake lakini anadai kila kitu kitakuwa sawa na mashabiki wataipata.
“Mimi siyo mtu wa filamu sana na ndiyo maana unaona najikita sana kwenye tamthilia, na nawashukuru mashabiki wangu kwani wanazipokea vizuri kazi zangu, pia hapo mwakani natarajia kuachia filamu yangu niliyoichezea sehemu hatari za kutisha,” alisema.
No comments:
Post a Comment