Thursday, December 13, 2012

FLAVIAN MATATA AZIDI KUIPA HESHIMA TANZANIA BAADA YA KUPATA TUZO YA "FACE OF AFRICA"

Mwanamitindo Flaviana Matata, weekend iliyopita ali update CV ya mambo ya urembo baada ya kufanikiwa kupata tuzo ya Face Of Africa kupitia African Diaspora Awards 2012, na kwa sababu hiyo kuzidi kuitangaza Tanzania kimataifa.

Tuzo hizi zilifanyika New-York Marekani jumamosi iliyopita , na lengo lake kuu ni kuwapongeza wa Africa wanaofanya mambo makubwa nje ya bara hilo.

Flaviana Matata mbali na kujihusisha na urembo pia ana 'Flaviana Matata Foundation' ambayo lengo lake kuu ni kusaidia katika mambo ya kijamii hasa wasichana, katika jitihada za kuwawezesha kielimu na kupunguza umasikini.

Toa maoni yako juu ya stori hii hapo chini.

No comments:

Post a Comment