SIKU chache baada ya kutangaza kuokoka, msanii wa filamu Bongo, Irene Uwoya amewaacha watu midomo wazi baada ya kutinga kivazi kilichoacha wazi maungo yake nyeti.
Tukio hilo lilijiri Jumatatu iliyopita katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar kwenye mkutano wa wasanii wa filamu na komedi ambapo licha ya kwamba ilikuwa mchana,Uwoya alitinga kivazi hicho chepesi ambacho kilisababisha sehemu nyeti kuonekana.
Hata hivyo, msanii huyo hakuonekana kuwa na wasiwasi kwani alikuwa akibadilisha mikao na kuacha nje sehemu yote ya mapaja hali iliyosababisha baadhi ya wasanii kuguna huku wakijiuliza ni kwa nini mwanadada huyo aliamua kuvaa nguo ya aina hiyo mchana kweupe.
No comments:
Post a Comment