Ile music video ya msanii Diamond Platnumz, ambao wimbo wake ulileta utata baina ya wasanii watatu, namaanisha H-Baba, Pasha na yeye Diamond, “Nataka kulewa” imekamilika na kilichobaki ni kuachiwa siku ya Jumapili ya wikiendi hii.
Kwa mujibu msanii Diamond na wa meneja wa msanii huyo Raqey ambaye ndiye alikuwa muongozaji mkuu wa utayarishaji wa video hiyo, kila kitu kimeshakamilika ikiwemo post production editing na sasa kilichobaki ni kuachiwa rasmi siku ya Jumapili katika Street Bash Party iliyoandaliwa na Clouds media kusherehekea kutimiza miaka 13 kwa kituo cha Radio ya Clouds FM.
No comments:
Post a Comment