Monday, December 17, 2012

Ferguson kumfuata Guardiola Marekani

LONDON, England
KOCHA wa Manchester United, Alex Ferguson wiki ijayo anatarajia kwenda mjini New York, Marekani huku uvumi ukikolea kwamba safari yake ni kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Pep Guardiola anayetajwa huenda akarithi mikoba ya kufundisha Dimba la Old Trafford.

Fergie anatarajia kuondoka Jumamosi baada ya mchezo dhidi ya Sunderland na huenda pia akatumia muda huo kufanya mazunguzo ya kibiashara na Big Apple akiwa kama balozi wa klabu nchini Marekani.
Ferguson anamiliki nyumba yake binafsi kwenye mji huo ambapo mtoto wake mkubwa Mark anaishi na wadogo zake eneo ambalo ni karibu na makazi ya kocha wa zamani wa Barcelona Guardiola, ambaye amepanga kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Kwa mujib wa habari za uhakika, tayari wawili hao walishakutana New York Septemba mwaka huu na kufanya mazungumzo ya awali kuhusu uwezekano wa kuchukua nafasi ya Fergie.

Amekuwa rafiki wa karibu wa Ferguson anayekwenda mjini New York kabla ya Guardiola, anayetajwa kuhitajika Arsenal ya England, hajaondoka kurudi Hispania kwa mapumziko ya sikukuu za majira ya mwisho wa mwaka. Wakati United imesema hakuna mazungumzo yoyote yatakayofanyika kati ya wawili hao wiki ijayo, kuna kila dalili kwamba watapata fursa ya kuonana kama ilivyokuwa Septemba.

No comments:

Post a Comment