Monday, December 17, 2012

Vibaka wa hatarisha maisha ya wanachuo wa vyuo vya CBE, Mwalimu Nyerere, Magogoni na IFM wanaokaa kigamboni.

Kundi la vibaka limeibuka maeneo ya kigamboni nakuanza kupora wanachuo waliopanga kigamboni. Kundi hilo ambalo linavamia usiku wa manane katika nyumba ambazo wanaishi wanachuo wa vyuo vya IFM, Mwalimu Nyerere, Magogoni na CBE na kuanza kuiba vitu vya wanachuo hao mbaya zaidi inafikia kipindi wanavamia mchana.

Habari vyuoni iliongea na mmoja wa wanachuo hao alisema kuwa kundi hilo ambalo huiba vitu vyao kama laptop, simu na subwoofer amesema “Ni kama mwezi sasa vitendo hivyo hutokea” pia aliongezea kuwa vibaka hao huvamia kwa kutumia mapanga. Wanachuo wengi sana mpaka sasa wamepoteza vitu vyao, aliongezea kuwa wamesha ripoti mara kibao kwenye kituo cha polisi kigamboni lakini hawaoni msaada wowote kutoka kwao.

Mwanachuo huyo aliongea kwa uchungu na kusema “tunnaomba polisi walifutilie swala hili kutokana kuwa tunapoteza vitu vyetu pia tunadhurika na jambo hili mpaka sasa ni wanachuo wengi sana tumepoteza vitu vyetu” pia maisha yao yapo hatarini kutokana na kitendo maana kila siku wanadhurika ambapo hali hiyo imekuwa tishio kwa wanachuo hao wanaishi maeneo ya kigamboni, alimalizia kwa kusema wanaomba msaada wa polisi kwaajili ya kulinda vitu vyao maisha yao kutokana wanakosa amani kwa jambo hili.

Kwa upande mwengine swala hili uongozi vya vyuo hivi unalaumiwa kwa kutojenga hosteli karibu na vyuo maana hosteli nyingi zilizopo mbali na vyuo huwa hazina ulinzi wa kutosha kwa wanachuo na mali zao. Tunaomba viongozi wa vyuo kuangalia suala hili kwa jicho la tatu ili kuepusha vitendo hivi kutokea kwa wanachuo pia wasimamizi wa hosteli au vyumba wanazopanga wanachuo ziwe na ulinzi wa kutosha.

No comments:

Post a Comment