Tuesday, December 4, 2012

RAYUU AZIPONDA FILAMU ZA WASANII WA BONGO MOVIE…

WAKATI wadau wakizidi kuzitoa kasoro filamu za bongo msanii Rayuu, amedai kuwa filamu nyingi zinazotengenezwa nchini hazina ubora na hazina mvuto wa mtu kuziangalia, zinaongoza kwa ubaya ni zile zinachezwa na wasanii wanaojiita bongo movie.

Ndani ya tasnia ya filamu Tanzania kuna makundi mawili na kati ya hayo lipo moja la wasanii wanaojiita bongo movie ambao wanajiona ni mastaa, pia kuna kundi lingine ambao si maarufu na ndilo linalojulikana kama wasanii wa filamu.

Kutokana na makundi hayo msanii huyo kwa upande wake alidai kuwa hayupo kwenye upande wa bongo movie, kwani kundi hilo limejaa majungu na wasanii wake wanajiona ni mastaa kuliko wengine huku wakisahau kuwa tasnia ya filamu ni moja.

Hata hivyo aliongeza kuwa uwepo wa filamu zisizo na ubora unatokana na hayo makundi kwani kila mtu anataka kutoa filamu kila siku bila kujua ubora wa kazi anayofanya na hii yote ni kutaka kushindani bila kujuavushindani huo unaharibu soko kwa sababu ya kazi zisizo na ubora.

“Mimi si msanii wa bongo movie na ukiniita hivyo utakuwa umekosea kuna kundi la wasanii ambao wanajiita bongo movie, lakini hata hivyo unaweza kuona filamu zao si nzuri kama za wasanii wengine ambao hutumia muda mrefu kutengeneza kazi moja, lakini wao kila baada ya wiki wanatoa filamu.” alisema.

Hata hivyo alisema kuwa ubaya wa kazi hizo unakuja pale unapokuta ndani ya filamu moja wamecheza watatu filamu nzima.


No comments:

Post a Comment