Monday, December 24, 2012

SAKATA LA MUME ALIYEMFUMANIA MKEWE AKIJIUZA

Mwanaume mmoja mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam, aliyejulikana kwa jina moja la Ombeni amemfuma laivu mkewe aitwaye Dina, akijiuza huku akidai kuwa mama watoto wake huyo kaacha kichanga nyumbani.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri katika Barabara ya Shekilango, maeneo ya Sinza, Dar usiku mnene wa saa 8:25 kuamkia Jumamosi iliyopita.

Ombeni alidai kuwa alifika nyumbani kwake Vijana-Kinondoni, majira ya saa 6:15 usiku akitokea safarini mikoani alikoenda kikazi takribani wiki mbili zilizopita ambapo alipoingia ndani aliwakuta wanaye wamelala bila mama yao.

“Nilimwamsha hausigeli, nikamuuliza mama yupo wapi? Ndiyo akanieleza kila kitu baada ya kumtishia kumfukuza kazi. Aliniambia siku hizi mke wangu anajiuza Barabara ya Shekilango,” alisema jamaa huyo.

Baada ya kujikusanyia data, ndipo alipowatafuta wanahabari ambao aliwaomba walifuate gari lake kwa nyuma kwani alikuwa akimsaka mkewe.


Haikuwa kazi rahisi kumpata mkewe kwani zoezi lilianza saa 7:05 hadi 8:25 usiku huku akifanya ‘ruti’ za kumwaga kutoka Shekilango hadi Mwenge na Mwenge hadi Shekilango.

Alipofanikiwa kumwona mkewe na kumwita kwa jina lake la Dina, ndipo akashtuka na kuanza kutoka nduki kisha kutokomea gizani akiwa na wenzake.

“Niliambiwa nikakataa, sasa nimeshuhudia kwa macho yangu, hakuna sababu ya kupindisha maneno. Nilimlipia mahari karibu ng’ombe tisa, atakapofika nyumbani ataikuta talaka ikimsubiri,” alisema Ombeni akionekana mwenye hasira.

No comments:

Post a Comment