Kwa mujibu wa Heka Heka ya leo katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, wanaume wengi wa kitanzania wanaoenda kutafuta maisha nchini Ubelgiji huishia kuwa mashoga ama kuolewa kabisa.
Kipindi hicho kimezungumza na watanzania waishio nchini humo ambao wamesema hali ni mbaya ambapo wanaume wengi huishia kuolewa ili kuwa na maisha mazuri na sehemu ya kuishi.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja, asilimia 85 ya wanaume wa Tanzania waishio nchini Ubelgiji huishia kujihusisha na vitendo hivyo hali iliyopelekea yeye ahame nchi hiyo na kwenda Marekani.
Ubelgiji ni nchi ya pili duniani kuhalalisha ndoa za jinsia moja mnamo mwaka 2003.Pia waziri mkuu wa nchi hiyo Elio di Rupo alikuwa kiongozi wa kwanza wa nchi za Jumuiya ya Ulaya kuapishwa kama shoga aliye wazi.
No comments:
Post a Comment