Mwandishi wa habari za michezo Shaffih Dauda ameripoti kwamba zoezi la klabu bingwa ya Tanzania bara Simba kupata mbadala wa beki wake aliyetimkia Yanga, Kelvin Yondani linaendelea baada ya Lino Musombo kutemwa na kusajiliwa kwa Keita na Ocheing ambao wameonekana kuhangaika kuziba pengo la Yondani, sasa klabu hiyo ya Simba inasemekana ipo katika harakati za kumrudisha mmoja wa mabeki wao bora katika kipindi cha miaka 10 iliyopita mganda Joseph Owino.
Simba ambao walianza ligi vizuri na kuongoza ligi kwa muda mrefu kabla ya kupoteza muelekeo mwishoni mwa raundi ya kwanza ya msimu wa VPL sasa katika kujaribu kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo ambayo imeonekana kuyumba sana msimu huu, uongozi wa Simba umeona bora ufanye mpango wa kumrudisha kundini Owino ambaye amesajiliwa Azam lakini amekuwa akikosa namba ya kudumu baada ya kurudi kutoka kwenye majeruhi yaliyomuweka nje kwa muda mrefu.
Taarifa ambazo hazijathibitishwa ni kwamba Simba tayari wapo kwenye mazungumzo na Azam ili kuweza kuona uwezekano wa kumsaini Owino ambae aliondoka Simba baada ya kupata majeraha ya goti ambayo yalimuweka nje kwa muda mrefu, na Azam wakamsajili akiwa mgonjwa wakamtibu lakini baada ya kupona amekuwa na urafiki mzuri na benchi la Chamazi.
No comments:
Post a Comment