MTOTO aliyejulikana kwa jina moja la Aneth (pichani) anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka miwili, mkazi wa eneo la Majengo Kaskazini jijini Mbeya ameunguzwa vibaya mwili wake na kulazimishwa kula kinyesi na Mama yake Mdogo aliyejitambulisha kwa jina la Revina.
Tukio hilo la kikatili liligundulika juzi eneo hilo majira ya saa tano asubuhi ambapo mwandishi wa habari hizi alifika eneo la tukio na kuukuta umati wa watu na mtuhumiwa akimuogesha mtoto huyo.
Mtoto huyo alipoulizwa kuwa ilikuwaje, aliongea kwa woga akisema kuwa alikuwa amefungwa mkono na kumwagiwa maji na kupigwa.Mtuhumiwa huyo alipohojiwa alikataa kusema chochote na kuishia kutaja jina lake moja la Revina, kisha wananchi wakaamua kumchukua mtoto huyo na mtuhumiwa na kuwapeleka kituo cha Polisi cha Kati.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa baada ya kutomuona mtoto huyo mwenye historia ya kuteswa na mama yake huyo mdogo anayeelezwa kuwa mama yake mzazi, Bahati Mkandara alifariki, wakaamua kumuuliza binti huyo ambapo aliwajibu kuwa mtoto huyo alikuwa kucheza na walipompiga ndipo akaamua kukimbilia chumbani na walipoingia wakamkuta mtoto amesimama akiwa uchi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Kaskazini, Shack Mwakanyamale alisema kuwa binti huyo amezoea kumtesa mtoto huyo huku mtoto wake akiwa na afya njema ambapo aliwatuliza wananchi wenye hasira kali na kuongoza msafara wa kumpeleka katika kituo cha polisi mtuhumiwa huyo.
No comments:
Post a Comment